GET /api/v0.1/hansard/entries/1419255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419255/?format=api",
"text_counter": 307,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mandago",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13577,
"legal_name": "Kiplagat Jackson Mandago",
"slug": "kiplagat-jackson-mandago"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii pia kuchangia Hoja ya Uwanja wa Manispaa ya Mombasa. Kwanza kabisa niseme mambo ya viwanja katika Taifa la Kenya ni ya muhimu sana. Nikichangia katika Hoja hii ya Sen. Faki ni kwamba, sio Uwanja wa Manispaa ya Mombasa pekee ambao umecheleweshwa. Katika Kaunti ya Uasin Gishu, tuko na uwanja wa kihistoria wa Kipchoge. Sehemu hiyo ndio imetoa wanariadha wengi waliobobea kwa michezo ya kimataifa na kuleta fahari nchi hii ya Kenya. Kwa hivyo, wakati tunakadiria jinsi Uwanja wa Manispaa wa Mombasa utashughulikiwa, pia viwanja vingine kama Uwanja wa Kipchoge Keino kule Eldoret, Kamarin kule Elgeiyo Marakwet County na pia Uwanja wa Kipchoge Keino kule Kapsabet, ni baadhi ya viwanja ambavyo vinafaa kuwa vimeshughulikiwa na Serikali. Pia isitoshe kuwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa itumie pesa iliyopewa kwa ugatuzi wa Mombasa kujaribu kuboresha huo uwanja. Mambo ya michezo ni ya muhimu sana kwa viwango vyote hasa vijana. Tukiweza kupata nafasi mahali pazuri pa kufanya michezo, vijana wetu watahepukana na mambo ya mihadarati na upotovu wa nidhamu katika muda ambao wangetumia kufanya michezo uwanjani. Ninaunga mkono Hoja hii na kusema kuwa wanapongojea fedha kutoka kwa Serikali Kuu hata wao kama Serikali ya Ugatuzi ya Mombasa waweze kuiweka kwa orodha ya kwanza kwa baadhi ya mambo ya maendeleo ambayo wanafaa kuyatekeleza kwenye kaunti yao. Naunga mkono."
}