GET /api/v0.1/hansard/entries/1419258/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419258,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419258/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kujibu hoja zilizotolewa na Maseneta kuhusiana na Hoja hii ya Kuidhinishwa kwa Ruzuku ya Masharti kwa Ujenzi wa Uwanja wa Munispaa ya Mombasa. Kwanza, ningependa kuwashukuru Maseneta wote ambao waliweza kuchangia Hoja hii: Sen. Madzayo, ambaye aliunga mkono wa kwanza, Sen. Maanzo, Sen. Cherarkey, Sen. Olekina, Sen. (Dr.) Khalwale, Sen. Beth Syengo, Sen. Mungatana, Sen. Omogeni, Sen. Oketch Gicheru, na mwisho, Sen. Mandago, ambao walichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Jambo la kufurahisha ni kwamba Hoja hii tumeizungumzia na kuichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Ni mara ya kwanza kwa Hoja kuletwa katika Bunge hili kwa lugha ya Kiswahili na kujadiliwa kwa Lugha ya Kiswahili mpaka ikakamilika. Ningependa pia kushukuru mchango wa Maseneta wote ambao wamechangia Hoja hii. Wamesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwanja wa kimataifa katika eneo ya Mombasa. Kwa mfano, sasa hivi, uwanja unaotumika wa Shirika la Bandari (KPA), lakini kwa sasa, wameufunga kwa sababu wanaufanyia marekebisho. Uwanja mwingine ambao unaweza kutumika na timu ya Bandari ni Uwanja wa Ukunda na Ukunda ni karibu kilomita 40 kutoka Jiji la Mombasa. Hali hii inaonyesha kwamba ipo dharura ya kukamilishwa kwa uwanja huu ili watu waweze kupata nafasi ya kuona michezo ya kimataifa. Vile vile, kushughulika na maswala mengine kwa sababu, uwanja sio wa mpira peke yake, lakina uwanja huu utakuwa na kidimbwi cha kuogelea, hall (auditorium) ya Sanaa. Kwa hivyo, ni uwanja ambao ni kamili kabisa. Swala lingine ni kwamba, sio kwamba Kaunti ya Mombasa haijaegeza hakika uwanja huu, lakini pesa zile ambazo wanaegeza kwa mfano katika bajeti ya mwaka 2023/24 waliweka Kshs80 milioni peke yake. Shilingi milioni 80 hazitoshi jambo lolote. Milioni 80 inatakikana zilipe askari wanaolinda pale na pia kulipia usafi katika uwanja ule. Hizo ni pesa ambazo itachukua zaidi ya miaka kumi au 20 kukamilisha ujenzi wa uwanja ule. Ningependa pia kuguzia maswala ambayo Sen. (Dr.) Khalwale ameyaguzia hapa kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa pesa Kshs500 milioni. Hakuna ushahidi wowote kuonyesha ya kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa fedha zikijumuisha kufikia Kshs500 milioni. Kwa sasa, Serikali kuu imepeleka wahandisi kutoka kwa Idara ya Public Works kuangalia na kutathmini ile kazi ambayo imefanyika pale. Wahandisi hawa wote wametoa ripoti ya kwamba kwa sasa hakuna pesa ambazo zimeweza kufujwa. Kwa hivyi, sio kweli kama alivyosema Sen. (Dr.) Khalwale wakati alipotoa machango wake mara ya kwanza na leo pia alipokuwa akiendelea kutoa mchango wake kusema kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa zaidi ya Kshs500 milioni. Ripoti zote za Mhasibu Mkuu, yaani Auditor-General, ambazo zimekuja katika Bunge hili, hakuna ripoti yoyote ambayo imesema ya kwamba kuna pesa Kshs500 milioni ambazo zimepotea katika uwanja wa Manispaa ya Mombasa. Kama Sen. (Dr.) Khalwale ana ripoti hiyo, kesho ailete katika Bunge hii ili tuiangalie na tuone kama pesa hizo zimebadhirishwa, basi tutaondoa Hoja hii ili kwanza tuangalie maswala ya pesa zilizopotea kabla ya kurudi hapa."
}