GET /api/v0.1/hansard/entries/1419264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419264,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419264/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, kauli niliyotoa ni kwamba jicho linaingia taka aka. Mhe. Bifwoli atakubaliana na mimi kuwa jicho linaweza kuingia kitakataka usiweze kuona sikusema takataka lakini kitakataka, yaani, particles kwa Kiingereza. Sen. Madzayo, fungua masikio wazi kwa sababu saa zingine maneno yataingia huku na kutoka kule. Uwanja huu hautafaidi Kaunti ya Mombasa pekee lakini utafaidi Pwani na nchi nzima. Hivi sasa tunapozungumza hatujui iwapo michezo ya Wabunge itafanyika wapi Mombasa. Hoteli tuko nazo lakini hatuna viwanja ambazo vinaweza andaa michezo kama hii. Huu ni wakati wa Serikali kunyoosha mkono kwa watu wa Pwani. Hivi sasa kuna maandalizi ya sherehe za Madaraka Day zitakazofanyika kwenye Kaunti ya Bungoma. Wanajenga uwanja ambao utaandaa sherehe hizo. Wanajenga State Lodge ambayo Rais atakaa akienda kuhudhuria sherehe hizi. Hii ni jukumu ya Serikali kwa sababu Serikali ni kama mwavuli mkubwa uliotufunika sote katika Jamhuri ya Kenya. Hatuwezi kuwa sehemu moja ina viwanja vingi. Hapa Nairobi kuna Nyayo Stadium, Kasarani na kiwanja kinachojengwa Talanta Stadium sehemu za Jamuhuri Park. Vile vile, kuna kiwanja cha kibinafsi cha jeshi la Ulinzi wa Kenya ambacho sisi kama wachezaji wa Bunge FC tunatumia kwa mazoezi. Bw. Spika wa Muda, ni muhimu tupate uwanja huu ili tusaidie talanta kwenye eneo la Pwani. Vijana wengi wamepotea kwa sababu ya mihadarati na itikadi kali, kwa sababu hawana fursa ya kufanya mazoezi na kuweka talanta zao uwanjani. Tunaomba tunapotamatisha Hoja hii kwa kutumia Kanuni ya Kudumu ya 66(3) ya Kanuni za Bunge hili, naomba tuairishe uamuzi wa kupiga kura hadi siku nyingine."
}