GET /api/v0.1/hansard/entries/1419493/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419493,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419493/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ", na pia National Treasury kuzuia pesa zinazokwenda katika kaunti zetu iwapo hawataweza kulipa madeni. Tumeona visa vingi vya serikali za kaunti kuomba pesa ili kulipa madeni, lakini wanapopata pesa zile wanatumia kufanya miradi ama wanatumia kwa safari zao, na hivi basi madeni yanaendelea kubakia na madeni haya yanazuia utenda kazi wa kaunti zetu. Wakenya wengi ambao wamefanya biashara na serikali za kaunti wamefilisika, mali yao imeuzwa na vile vile wamekuwa hawawezi kufanya biashara na hivyo basi, pesa nyingi na mali imepotea kutokana na ukosefu wa uadilifu katika serikali za kaunti. Marekebisho haya yataweka meno ambayo yatasaidia kuuma wakati kutakuwa na upungufu iwapo hawataweza kulipa madeni hayo kwa muda unaofaa. Bw. Spika, ninaunga Mkono."
}