GET /api/v0.1/hansard/entries/1419605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419605,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419605/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa hii fursa ambayo umenipa ili niuinge mkono huu Mswada ulioletwa kwenye Seneti na Sen. Ogola kuhusu afya ya mama wajawaaztio, waliojifunugua na watoto waliozaliwa. Kumekuwa na sheria nyingi ambazo zimetungwa kuangazia haya maswala na pia kuna sera zingine ambazo hazijawekwa katika sheria. Katika hekima ya Sen. Ogola akaona ni vyema alete Mswada huu wa kuangazia hayo maswala. Bw. Spika wa Muda, nitaangazia vifungu kama tano hivi. Ya kwanza ikiwa ni Kifungu cha tano ambacho kinaangalia haki ya matibabu vile ilivyoangaziwa katika Ibara ya 43 kwamba kila mwananchi au Mkenya kulingana na Katiba anahitaji kuyafikia matibabu. Mama mjamzito, mama aliyejifungua na mtoto mchanga wana haki za kupata matibabu na huduma ya kwanza inayopelekea kuafikia hii afya. Kifungu cha sita kinasema kuwa mwanamke ambaye hana mimba anafaa kupata huduma fulani. Kuna huduma ya aina mbali. Kwa mfano, kuna maelezo ya vyakula ambavyo mwanamke ambaye hana mimba-mwanamke ambaye hana mimba basi si mama-anafaa kula."
}