GET /api/v0.1/hansard/entries/1419608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419608/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Sen. Ogola ameona ni vizuri tuiangazie afya ya mama na mtoto. Pia ni lazima tuimarishe afya ya mwamamke asiye na mimba ili apate hamasa ya kutosha. Ikifika wakati anapopendelea kuwa na mtoto aliye na afya nzuri basi kabla ya kuenda kwa tendo litakalo pelekea kuwa na mimba awe amechunguzwa vizuri. Kifungu cha saba kinaangalia huduma zinazofaa kupewa mwanamke aliye na mimba. Kila wakati kwenye mafunzo ya kiafya na maelezo ya redio na vyombo tofauti vya habari, taarifa inasisitiza na kueleza vyakula na dawa ambazo zimepigwa marufuku kwa wajawazito. Zaidi ya hayo, pia kuna vinywaji ambavyo kama mja mzito huwezi kutumia. Kwa hivyo haya ni mambo ambayo yamekuwa lakini Mswada huu umeelezea ni vyema mama aliye na mimba apate haya maelezo. Bw. Spika wa Muda, mambo mengine yanayofaa kuelezewa mama mja mzito ni kazi amabazo anafaa kufanya na kadhalika pamoja na kuenda kupokea huduma za kliniki. Kifungu cha saba pia kinaangazia maswala ya mama aliye na mimba. Sheria hii inafaa kuangalia mambo ya huduma za dharura. Ni vyema kuwe na mpango dhabiti au mufti wa kuhakikisha kwamba mja mzito atajifunga kwa hali isiyo tatanishi. Kule nyumbani na pia katika maisha yangu nimeona vituko vya mama mjamzito anayetaka kujifungua lakini hakuna vifaa au huduma za kutosha ili kuhakiksha kuwa mama aliye na dharura anaweza fika hospitalini. Mwaka wa 1999, nikiwa naendesha gari, kuna mama ambaye alijifungua kwa gari langu kwa sababu nilimpata barabarani. Hakukuwa na ambulance na simu wakati huo. Ilibidi nimbebe na kabla hajafika hospitalini, akajifungua. Ilikuwa ni hali ya hatari sana kwa sababu sikuweza kumsaidia huyu mama kujifungua. Bw. Spika wa Muda, kujitayarisha na kuwapa mama wajawazito elimu ya kutosha ni muhimu sana. Juzi tu, miaka miwili iliyopita, kuna mama mja mzito alipelekwa kwa"
}