GET /api/v0.1/hansard/entries/1419610/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419610,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419610/?format=api",
    "text_counter": 311,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "kule Voi, ambayo haikuwa na vifaa vya kutosha. Alivyoanza kujifungua, kwa bahati mbaya, mtoto alianza kuja visivyo stahili. Alikuja miguu ikiwa imetangulia. Inatakiwa mtoto aje na kichwa mama anapojifungua. Hawa nurses walipiga simu kwa kituo cha Referral cha Moi kwa mfano na wakaambiwa kwamba, ambulance itakuja. Walingoja kwa masaa matatu bila ambulance kufika. Kwa bahati nzuri, huyu mama, alisaidiwa na hao madaktari na akajifungua kwa miujiza. Kwa hivyo, inatakiwa kutojitayarisha vya kutosha kuwasaidia akina mama wajawazito kujifungua iwe ni kosa la uhaini ama criminal offence. Tumeona hali ya afya imedorora katika hospitali zetu. Kwa mfano, itakuwaje mama angojee masaa matatu bila kufikiwa na ambulance ? Ile procedure inatakiwa ni kwamba; mama akijitayarisha kujifungua, basi kuwe na ambulance, na wakati ambulance imeitishwa, isichukuwe dakika 30 kabla haijafika. Na wale ambao wanamhudumia mgonjwa, wawe tayari wametayarisha kufanya upasuaji kwa huyu mama ili kumsaidia. Mheshimiwa Beatrice, tufanye mageuzi ili kutojitayarisha vya kutosha kwa mahospitali na county governments liwe ni kosa la jinai. Hii ni kwa sababu, akina mama na watoto wengi ambao wanakufa wakati wa kuzaliwa ni kwa sababu ya matayarisho ambayo hayafai. Kwa kimombo ni medical negligence . Bw. Spika wa Muda, hii sehemu ya nane inaangazia huduma za mama na mtoto wakati amezaliwa. Kumekuwa na matibabu ya bure katika hospitali nyingi. Lakini kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}