GET /api/v0.1/hansard/entries/1419611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419611,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419611/?format=api",
    "text_counter": 312,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "sasa, hali ya afya imedorora katika kaunti zingine. Unapata ya kwamba, matibabu ya mtoto mdogo ambaye amezaliwa ni ya bure lakini, bado wanalipia kitanda. Kwa hivyo, watu wengi wanaogopa kuwapeleka watoto wao hospitalini kwa sababu ya kutozwa pesa na wakati mwingine, hao watoto wanakufa. Nilikuwa na mfanyikazi wangu mmoja ambaye alikuwa na mtoto mgonjwa; akampeleka hospitalini na akashindwa kumtoa kwa sababu licha ya kuwa kuna mpangilio wa Linda Mama na sera za sheria zimewekwa na serikali za kusaidia watoto kama hawa, alikosa kutolewa kwa sababu ya bill ya Kshs4,500 kitanda na chakula pekee yake. Kwa hivyo, kukiwa kunatengenezwa kanuni za kuwezesha huu Mswada kufanya kazi, basi iwe bayana ya kwamba kama huduma ya matibabu ya mtoto aliyezaliwa hadi miaka tano ni bure, iwe bure bin bure ama bure ya bure kabisa. Hii ni kwa sababu, hata chakula na kitanda bado ni malipo na watu wengi hawawezi kumudu.Nakubaliana na wasemaji ambao wamesema mbele yangu kwamba, hii programme ya Linda Mama ilikuwa nzuri. Lakini Serikali yetu imetoa huduma nyingi sana na naogopa hata hii huduma ya Linda Mama inaweza ondolewa pia. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, tukiangalia wanafunzi wa shule za upili walikuwa wanapata matibabu ya bure. Saa hizi, hiyo imeondolewa na sasa wanalipa. Kuna sera zingine nzuri zimekuweko na saa hizi zimetolewa. Ni vizuri hii ya Linda Mama ibaki hapo. Jambo la mwisho ni sehemu ya 12 ambayo imeangazia majukumu ya Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Katika hii sheria, majukumu ya Serikali ya Kitaifa yamekua ni kuunda sera za kuelekeza vile huu Mswada utakavyotekelezwa. Katika serikali za magatuzi, yametoa njia na mbinu za kuhakikisha kwamba huu Mswada unatekelezwa vilivyo. Bw. Spika wa Muda, hatuwezi tekeleza huu Mswada vyema na vilivyo kama hatutakua na pesa ya kutosha katika magatuzi. Ninafurahi kwa sababu, wakati wa kupitisha Mswada wa Division of Revenue Bill, Maseneta walikubaliana pesa ziongezwe mpaka shilingi bilioni Kshs415. Ninashukuru wenzangu wa upande ule mwingine kwa sababu, mwaka ule uliopita, hatukukubaliana kwa ile pesa inayotakikana kupelekwa kwa yale magatuzi na wakapiga kura pesa kidogo iende. Lakini saa hizi, moja kwa moja, tumeweza kukubaliana ile pesa inayoenda kwa magatuzi ni muhimu na sisi kama Maseneta tunaopigania na kulinda ugatuzi, tupigie kura pesa nyingi zaidi ili ziende kwa kaunti zetu. Hii ni kwa sababu, Miswada kama hii ni ya kuhakikisha ile ibara ya 43 ya kuhakikisha kwamba huduma za afya zimefikia wananchi wetu, zinawafikia bila kukosa. Lakini, Bw. Spika wa Muda, kuna kucheleweshwa kwa pesa zile za kaunti kwenda kwa magatuzi inayopelekea ile miradi ya maendeleo ama zile programmes zinazowezesha miswada kama hii kutekelezwa kuwa na shida kubwa saa zingine. Hii ni kwa sababu, sheria inasema kabla mradi hujaanzishwa, kuwe kuna pesa tayari katika akaunti. Lakini kama pesa zitakua zinachelewa kwenda kwa magatuzi, basi Miswada kama hii na huduma kama hizi zitakua ngumu kufikia wananchi wetu. Ninasema tuunge huu Mswada mkono na pia upigwe msasa kidogo pale unapotakikana kupigwa msasa ili kuurotubisha zaidi na pia tuupitishe. Huu Mswada ukienda kule Bunge la Kitaifa, tuupigia debe pia ili upite. Asante, kwa hii fursa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}