GET /api/v0.1/hansard/entries/1420201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420201,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420201/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Mwenyekiti. Katika Kifungu cha 19 (a), kuna maelezo bayana kwamba halmashauri hii itaweza kuwapa kibali wakulima wa miwa, iwapo wataelekeza ama wataeleza kwa mapana na marefu kwamba hawana mkataba wowote na kiwanda chochote katika eneo lao. Basi watapewa ruhusa kuendeleza na mkataba ambao uko katika eneo lingine. Vile vile, jinsi Seneta wa Narok amesema, iwapo hauna deni na kiwanda ama kongamano la wakulima, utaweza kupewa nafasi na hakuna stakabadhi yoyote inayoonyesha kwamba una mkataba wowote. Zaidi ya hapo, Kifungu cha 19(b), inaeleza bayana kwamba mkulima atapewa nafasi ya kupewa ruhusa na halmashauri hii iwapo kandarasi yake imekiukwa na msagaji wa sukari. Hivi kwamba, halmashauri itapea mkulima ruhusa kuuza miwa yake kwingine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}