GET /api/v0.1/hansard/entries/1420202/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420202,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420202/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Mkulima ama halmashauri itathibitisha kwamba kiwango ama miwa inayopatikana katika eneo hilo imezidi kiwango cha msagaji wa miwa kudhibiti. Hivyo, wakulima watapewa nafasi ya kuuza miwa yao katika kiwanda kingine katika eneo lingine. Mwisho, kiwanda ambacho anataraji kupeana miwa kiko katika eneo lingine na ana mkataba. Sasa hayo yote yataweza kuafiki yale ambayo Sen. (Dr.) Oburu alikuwa anaangazia, ili kwamba mkulima asifinywe na vile vile mikataba kati ya mkulima na kiwanda ama kiwanda na kingine, kila mwekezaji afanye jinsi sheria inavyostahili. Asante."
}