GET /api/v0.1/hansard/entries/1420631/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420631,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420631/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili nichangie huu Hoja hii iliyoletwa na Senata wa Narok, Ledama Olekina, kuhusu malipo ya wanakandarasi ambao wamefanya kazi kwa serikali zetu za kaunti. Ukiangalia Hoja hii, hali ilivyo katika kaunti zetu ni kwamba kuna wanakandarasi wengi wamefanya kazi lakini hawajalipwa. Hili limepelekea hawa wanakandarasi kufunga biashara zao, wengine kujiua na benki nyingi sasa kukataa kuwapa mikopo wakandarasi wanaofanya kazi na serikali za kaunti. Hii imepelekea umaskini mwingi kwa wanakandarasi. Nakubaliana moja kwa moja ya kwamba ni vyema sheria ifuatwe wakati tunalipa wakandarasi kwa sababu sheria inasema kwamba wakati tumeanza mwaka mpya wa pesa, zile pesa za pending bills ziwe za kwanza kulipwa katika pesa zote zitakayoenda kwa serikali za kaunti. Bw. Spika, ufisadi ndio unaleta ukosefu wa kutolipwa kwa wanakandarasi. Hii ni kwa sababu nchini Kenya kuna jambo ambalo linaitwa asilimia kumi ama watu kutaka hongo ili kupeana kandarasi. Watu wengi katika kaunti zetu huwa wamepata pesa tayari kwa zile kandarasi zimefanyika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}