GET /api/v0.1/hansard/entries/1420632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1420632,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420632/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Na wakati wamepata pesa za kaunti badala kulipa wanakandarasi, wanatumia zile pesa ili kupeana zabuni mpya ili wapate asilimia kumi. Hii imepelekea malimbikizi ya pesa ambazo zinatakikana kulipwa wanakandarasi. Pesa hizi ni zaidi ya bilioni mia moja na saba zinazodaiwa Kaunti ya Nairobi. Kiambu ni shilingi bilioni tano nukta saba, Mombasa ni shilingi bilioni tatu nukta tisa na Taita-Taveta ni shilingi bilioni moja nukta mbili. Jambo la kushangaza ni kwamba hata wakati gatuzi zetu zinasema kwamba zimeweka katika bajeti pesa za kulipa wanakandarasi, pending bills au muswada unaosubiri haupungui. Taita-Taveta, kwa mfano, mwaka uliopita wa 2022/2023, walilipa shilingi milioni mia tatu hamsini. Lakini badala ya muswada unaosubiri kupungua unaongezeka. Kwa hivyo, nakubaliana na mapendekezo yaliyoko katika Hoja hii ya kwamba Mdhibiti wa Bajeti aangalie kwa ukaribu bili zilizosalia zinazolipwa na pesa ambazo anapitisha. Iwapo kaunti haijalipa muswada unaosuburi au bili zilizosalia, wasipewe pesa katika ule mgao uanofuata. Kuna kitu tunaona katika kaunti zetu. Kwa kimombo inaitwa"
}