GET /api/v0.1/hansard/entries/1420689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420689,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420689/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "kama ushuru na raia wa nchi hii. Pesa za kaunti sio pesa ambazo hazina hesabu, ziko na hesabu yake na zinatakiwa kujulikana zimefanya kazi gani. Bw. Naibu Spika, kuna jambo linalojulikana kama public participation . Kabla mradi haujapitishwa katika bunge la kaunti, lazima wananchi waseme mradi wanaotaka na mahali utafanyika. Baada ya wananchi kuamua mradi wanaotaka ufanywe, wanaanza kupanga mpango wa kuanza mchoro kama ni mjengo au barabara. Halafu, huo mchoro unawekewa bei katika shughuli inayoitwa quantity survey . Baada ya gharama ya ujensi huo kujulikana, inapelekwa katika bunge la kaunti na kushughulikiwa ipasavyo. Baadaye, inapitishwa kama mpango ambao umetoka kwa wananchi wa kaunti hiyo. Baadaye, mambo ya vile kazi itafanyika inatangazwa katika magazeti. Majina ya"
}