GET /api/v0.1/hansard/entries/1420705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1420705,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420705/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "msaada huko. Ile pesa inabaki huko ni ile ya watu wa kuteremsha hiyo mizigo wanalipwa, peke yake. Bw. Naibu wa Spika, kama ni shilingi mia mbili, ile pesa inabaki huko, ni shilingi elfu kumi ya kuteremsha hiyo mizigo peke yake na shilingi 199,990,000 inarudi hapa Nairobi. Hata pesa hakuna kwa miji kwa sababu pesa zote zimerudi Nairobi, vile imetumwa kutoka Nairobi, inarudi Nairobi. Lakini wale watu masikini kidogo wako na milioni moja au mbili; na wamefanya kazi na kaunti, mpaka leo, miaka tano au sita baadaye, hawajapata pesa zao. Ningependa hata Mhe. Rais wetu, akae afikirie raia wake, kwa sababu nchi zingine za Ulaya ama Saudi Arabia, wale wanaopanda ngano huko Saudi Arabia, serikali inawapa msaada. Kama ngano ingekuwa ni shilingi elfu moja, serikali itawapa shilingi mia mbili ili wauze ngano yao, shilingi elfu moja, mia mbili. Bw. Naibu wa Spika, lakini serikali yetu inaiba kutokwa kwa raia wa Kenya. Raia anapatia serikali deni na serikali hailipi deni. Saa hio serikali ya nchi nyingine inasaidia raia wake na hii ya Kenya inamaliza raia wake. Sen. Olekina amefanya kazi nzuri sana na ninaunga mkono. Ikiwezekana, tuweke sheria ya kwamba, hakuna maendeleo yatafanyika katika makaunti ama hata kwa nchi, mpaka wale watu wanalia kwa saa hii walipwe pesa zao. Nikimalizia, ukiangalia makaunti, kuna watu wanafanya kazi kwa niaba ya magavana wa hizo kaunti. Kampuni zingine zikifanya kazi, zinalipwa pesa hata kwa muda wa wiki moja. Wale raia wa kawaida wanaenda kujaza tenda na wakijaza hizo tenda, wanaenda kutafuta pesa zao na hawapati hizo pesa hata kwa miaka kumi. Hizi kampuni ni kubwa na zinafanya kazi ya milioni mia mbili, tatu au nne. Majina yao yanatakikana yaletwe mbele ya Seneti wafanyiwe uchunguzi. Kuna watu wanaandikisha makampuni leo na kesho yake, wanajaza tenda ya kaunti. Siku ya tatu, anapewa kazi ya milioni mia mbili na baada ya wiki mbili, analipwa pesa. Bw. Naibu wa Spika, hio pesa baada ya wiki mbili, inatoka kwa hio akaunti na haijulikani mahali inaenda. Inatakikana hata hawa watu wachunguzwe hiyo kazi yao walianza lini na walifanya na kampuni gani na imetoka hiyo akaunti ikaenda akaunti gani."
}