GET /api/v0.1/hansard/entries/1420773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1420773,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420773/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aisha Jumwa",
    "speaker_title": "The Cabinet Secretary for Gender, Culture, the Arts and Heritage",
    "speaker": {
        "id": 691,
        "legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
        "slug": "aisha-jumwa-katana"
    },
    "content": "Mhe. Seneta wa Nairobi, Sen. Sifuna sisi pia wakati mwingine tunaelewa majukumu ya Serikali Kuu na serikali za ugatuzi. Ukweli ni ukweli na hauwezi kubadilika. Kwa hivyo, hivyo ndivyo ilivyo. Kwa maktaba kuu ambayo ofisi yangu iko pale kama Waziri wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi, nataka niseme ya kwamba tumekuwa na mazungumzo ya kutosha na ya kina pamoja na Baraza la Magavana na tuna makubaliano ambayo tunaenda kuafikiana. Hii ni kwa sababu ya yale niliyotangulia kuyasema, kwamba, maktaba kuu za kitaifa zinahifadhi kumbukumbu nyingi za masuala ya kitaifa. Kwa hivyo, tuko na maktaba tatu, sio Maktaba Kuu pekee yake. Hapa Nairobi tuko na Maktaba Kuu, Maktaba ya Buruburu na ya Nakuru Kaunti ambazo bado ziko katika mikono ya Serikali kuu chini ya Wizara hii ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi. Kwa hivyo, mazungumzo bado yanaendelea. Leo siwezi nikakupa jibu mwafaka ya kwamba wiki ijayo tutaenda kuwachilia huduma hii muhimu iwe katika mikono ya serikali ya Kaunti ya Nairobi. Lakini, punde tu tutakapo afikiana, labda nitarudi hapa kuwapa ripoti kamili. Asante."
}