GET /api/v0.1/hansard/entries/1420788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420788,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420788/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Namkaribisha Bi. Waziri. Najulisha Seneti ya kwamba, katika Kamati yetu ya Labour and Social Welfare, tuko na mapendekezo ya Mswada wa usimamizi wa maktaba zetu. Mswada huu umependekezwa na Seneta, Kamishina, Mhe. Joyce Korir. Baada ya kujulishwa kwamba jukumu hili limegatuliwa kwa gatuzi zetu, na hili ni ombi Bi. Waziri, kwa sababu umejieleza vizuri kwamba usimamizi pamoja na raslimali za kusimamia maktaba hizi umeenda katika gatuzi, ni muhimu kama Serikali kuu, muweze kuangalia kwa sababu maktaba hizi zimebaki kama mahame. Katika Kaunti ya Mombasa, kuna moja ambayo ni mzee. Hata vitabu vilivyo pale vinakaa kuchoka. Tusikwepe majukumu kwa kusema kuwa maktaba zimegatuliwa. Tushirikiane na magavana kuona kwamba malengo ya kuwa na maktaba yameafikiwa. Maktaba zinafaa kuboreshwa. Shughuli zinazoendeshwa katika maktaba hizo ziwe ni za kumfaidi Mkenya. Wengi wataona kuwa majukumu yameenda na kurudi kule. Cha muhimu zaidi kwa mwananchi ni huduma nzuri katika taasisi zetu. Bw. Naibu wa Spika, kama wengine walivyosema, natoa shukran zangu kwa Bi. Waziri kuweza kufika hapa."
}