GET /api/v0.1/hansard/entries/1420989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1420989,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1420989/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na mambo ya mazingira. Mazingira ni muhimu na tunaelewa kuwa uharibifu wa mazingira unaleta magonjwa na mambo mengi ya hasara kwa binadamu. Lakini NEMA wako na tabia ya kutoa leseni kiholela bila kufikiria mikakati ambayo ingewekwa kudhibiti yale madhara yangeletwa na ule mradi unaoanzishwa. Hatukatai miradi kwenye nchi na waekezaji, lakini tunasema NEMA iwajibike kuthibitisha kwamba, ikiwa watatoa leseni kwa mradi wowote, wahakikishe pia wameweka mipango ya kuzuia athari na ajali za ule mradi utakaoletwa ile usidhuru watu. Bw. Naibu wa Spika, kwa hayo machache, nashukuru sana kwa huu muda mfupi."
}