GET /api/v0.1/hansard/entries/1421000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421000/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Thank you, Mr. Deputy Speaker. I will be very brief. Ningependa kuchangia Taarifa ambayo umeileta hapa kama Seneta wa Meru kuhusu kutekwa nyara na hatimaye kuuwawa kwa mwanablogu Snipper. Ni jambo la kusikitisha kwamba hivi sasa ambapo tunayo Serikali ya Kenya Kwanza iliyo mpya, watu bado wanauliwa kiholela. Hili jambo la kuuwa watu kiholela limekuwa likitokea na serikali zilizopita, ila sasa donda hili sugu halijaweza kutibiwa na wananchi wa Kenya kuishi kwa amani kama Katiba inavyosema. Majuzi pia kuna mtu mmoja mjini Mombasa aliyeitwa Yusuf Swaleh Ahmed Kandereni au Candy Rain aliyekuwa ni mfanyibiashara Mombasa. Alitekwa nyara na polisi nyumbani kwake, akapotea na baada ya siku nane maiti yake ikapatikana sehemu inayoitwa Kuruwitu katika Kaunti ya Kilifi. Habari zilizoko ni kwamba alitekwa nyara na polisi kisha kuuliwa kwa tuhuma kwamba alikuwa mmoja wa wale wanaouza mihadarati. Bw. Naibu wa Spika, ni wazi kwamba nchi yetu ya Kenya ina mahakama ambazo zina uwezo wa kufanya kesi yoyote katika nchi. Je, ni sawa kwamba polisi hadi sasa hawajeweza kutoa taarifa yoyote kuhusiana na tuhuma hizo kwamba walihusika katika mauaji ya Kandereni au Candy Rain? Ni wazi kuwa kunyamaza kwa polisi ni kuwa wanajua ni kitu gani walifanya. Hii ni kuendelea kwa mauaji ya kiholela ambayo Serikali hii ilikuwa imesema litakuwa ni jambo la kusahau."
}