GET /api/v0.1/hansard/entries/1421080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421080/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kujibu Hoja hii ambayo ni muhimu sana katika Bunge letu la Seneti pamoja na Bunge la Kitaifa kwa ujumla. Kwanza, ninawapongeza na kuwashukuru Maseneta wote ambao wamechangia Hoja hii wakiongozwa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili; Sen. Cheruiyot, Sen. Sifuna, Sen. Olekina, Sen. Orwoba na Sen. Oketch Gicheru, ambaye pia ni mwanachama wa Kamati ya Fedha na Bajeti; Sen. Maanzo, Sen. Kisang’, Sen. Tobiko ambaye amezungumza kwa hamasa kubwa, Sen. Mandago ambaye alikuwa Gavana wa Gatuzi la Uasin Gishu na mwisho, Sen. Osotsi. La msingi ni kuwa, ijapokuwa dhiki ya deni imepungua kwa sasa lakini bado kuna hatari ya dhiki hiyo kurejea tena. Kwa sababu tumeona kuwa Serikali ilisema kwamba italipa deni la Eurobond kufikia Disemba mwaka uliopita lakini hawakuweza kulipa na walipopata mkopo mwingine mwezi wa pili, ulikuwa ni mkopo wa US$1.5 billion ilhali deni la Eurobond ni US$2 billion. Kwa hivyo, ijapokuwa malipo yatafanywa kwa wakati, lakini swala la dhiki ya deni yaani debt stress ni kitu ambacho kitaendelea kuwa katika shingo letu kwa muda mrefu utakaokuja. Mapendekezo yaliyotolewa na Maseneta wote ni mapendekezo ya kufaa kuhusiana na vipi bajeti yetu itakavyokuwa. Tumeona kuwa kutakuwa na upungufu wa Kshs703.9 bilioni katika bajeti ya mwaka huu. Upungufu huo utafadhiliwa na madeni ya kutoka nje ya asilimia 55. na vile vile madeni ya kutoka ndani ya asilimia 45. Katika madeni yatokayo ndani, Serikali itakuwa inapingana na wananchi pamoja na wafanyibiashara kupata pesa za kufanya maendeleo ama kuziba pengo lililoko na hiyo itasabisha mkurupuko wa riba katika nchi yetu. Vile vile mkurupuko huo utazidi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}