GET /api/v0.1/hansard/entries/1421083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421083,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421083/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "lakini hayo sio kweli kwa sababu tumeweza kujadili mapendekezo yote na kuyaweka katika Ripoti ile na kwamba hatukuweza kulichukua pendekezo hilo kama pendekezo la Kamati sio kwa lengo la kuyapuuza mapendekezo ambayo yametolewa. Suala la ufadhili wa kutoka kwa watu binafsi yaani public-private partnership ni suala ambalo tumejadili hata katika Bunge lililopita. Wakati tulipokuwa tunaangalia mabadiliko ya debt ceiling yaani mabadiliko ya juu ya deni, tuliangalia masuala ambayo Serikali ilikuwa imependekeza. Mojawapo ya pendekezo ambalo lilitolewa na Serikali ni kwamba walikuwa wamepitisha sheria ya ile public private partnership na ya kwamba sasa miradi ya Serikali inapelekwa katika misingi ya public-private partnership kuangalia kama wanaweza kupata mfadhili wa kufanya mradi ule ili waweze kumlipa pole pole. TheNairobi Expressway ni moja ya miradi ambayo imeweza kufanyika na ni kweli tunaweza kusema ya kwamba ni mradi ambao umeweza kufaulu kwa sababu tumeona malengo yametimia na wananchi wanalipa bila kulalamika kwa njia yoyote. Cha kustaadhabisha ni kuwa Serikali hii ilipochukuwa mamlaka ilijaribu kupuuza ile miradi na mikakati yote ya nyuma ambayo ilikuwa imewekwa kuhakikisha kwamba ile sheria imeweza kutumika kuwafaidi wananchi. Bw. Spika wa Muda, nimefurahi kwa sababu Serikali inajaribu kuchukua mbinu hii ya kuleta maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Hii njia itasaidia kupunguza pressure ambayo inatokana na upungufu wa fedha ambazo Serikali inayo kwa sasa na kuhakikisha tumepata maendeleo. Miradi mingi inaweza kufanywa kwa njia hii ya ufadhili wa kibinafsi ili kupunguza madeni na kuweka pesa katika nyanja za kuzalisha kwa haraka zaidi kuliko zinazozalishwa kwa miradi inayochukua muda mrefu"
}