GET /api/v0.1/hansard/entries/1421090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421090,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421090/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Lazima orodha hii ya madeni ije hapa ili tuangalie lika deni lilichukuliwa kwa mradi gani na tujue pesa zilizochukuliwa kwa niaba ya Wakenya zilitumika aje. Kulikuwa na tuhuma hapa kwamba Eurobond ya kwanza ilipochukuliwa pesa hazikuja katika nchi ya Kenya. Tuhuma hizo hazikuweza kujibiwa. Kwa hivyo iwapo tutaiona orodha ya madeni tutaamua kwamba je ililetwa nchini au la? Mwisho ni kuwa Maseneta pia wamezungumzia maswala ya ufisadi. Hatuwezi kuufungia macho ufisadi kwa sababu ni kitu ambacho kinaathiri Serikali Kuu na serikali zetu za kaunti. Serikali nyingi za kaunti zina malimbukizi ya madeni kwa sababu hawajaweza kulipa wanakandarasi kwa wakati unaofaa. Hii inasababisha kucheleweshwa kwa maendeleo katika kaunti zetu na kulimbikizwa kwa madeni kila mwaka nenda mwaka rudi. Bw. Spika wa Muda, asubuhi Waziri wa Barabara na Uchukuzi alikuwa hapa na alisema kuwa Wizara yake ina madeni ya Ksh150 bilioni kwa masuala ya barabara pekee kwenye Kenya National Highways Authority (KeNHA) Kenya Urban Roads Authority (KURA) na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) ambayo inadaiwa. Hii ina maana kuwa kila mwaka tutakuwa tunalumbukiza madeni ambayo hayatasaidia. Jambo la kwanza ambalo pato la Serikali linastahili kufanya ni kulipa deni. Ikiwa madeni ni mengi ina maana kwamba pesa za maendeleo zitapungua. Hii ina maana kwamba hatutapata maendeleo ambayo tunatarajia katika nchi yetu. Ni lazima Serikali hii ijitolee kupambana na ufisadi. Ishara ambazo Serikali imetoa mpaka sasa ni kwamba hawako tayari kupambana na ufisadi. Kesi nyingi ambazo zilikuwa zimepelekwa mahakamani zimeondolewa. Hii inawavunja moyo wale wachunguzi wa kesi hizi za ufisadi. Iwapo watapata nafasi nyingine ya kufanya uchunguzi, sidhani watakuwa na hamu na ghamu ya kufanya uchunguzi ule ili kuhakikisha ya kwamba wale ambao wanatuhumiwa wamepelekwa mahakamani na hatimaye kupatikana na hatia. Kwa hayo mengi, nashukuru Bunge hili kwa kutupa fursa ya kuleta Ripoti hii muhimu katika mfumo wa fedha wa nchi yetu. Asante."
}