GET /api/v0.1/hansard/entries/1421169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1421169,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421169/?format=api",
    "text_counter": 54,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kingi",
    "speaker_title": "The Speaker",
    "speaker": null,
    "content": "Ngoja nikueleze. Pengine nifafanue ili uelewe. Kweli Waziri aliye mbele ya Seneti hivi leo ni Waziri wa Barabara, Uchukuzi na Makao. Haimaanishi kuwa utauliza swali lolote lile linalogusia barabara. Utauliza swali ambalo lina uhusiano na lile Swali la mwanzo ambalo limeulizwa na Mhe. Sen. Enock. Kwa sababu ukichagua barabara yoyote ama swala lolote ambalo linaguzia barabara, hilo swali litakuwa tofauti kabisa na lile swali ambalo limeulizwa na Sen. Wambua. Endelea, Sen. Munyi Mundigi"
}