GET /api/v0.1/hansard/entries/1421179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1421179,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421179/?format=api",
    "text_counter": 64,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kipchumba Murkomen",
    "speaker_title": "The Cabinet Secretary for Roads and Transport",
    "speaker": {
        "id": 440,
        "legal_name": "Onesimus Kipchumba Murkomen",
        "slug": "kipchumba-murkomen"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kusema kwamba hilo swali la Sen. Munyi Mundigi ni swali la maana sana. Tuko na nia ya kupanua barabara zetu zote kutoka Mombasa mpaka Malaba, kutoka hapa Museum Hill mpaka Moyale na pia kutoka Makutano kama vile Mhe. Mundigi amesema, mpaka ifike Meru, ipite Timau ikutane na ile barabara ya kuelekea Isiolo. Pia, tuna mipango ya kupanua barabara ya kutoka Isebania iende mpaka kwa mpaka wetu na ndugu zetu kutoka Sudan Kusini. Hilo swali ni la maana, lakini hivi punde, nitarudi na Mswada wa kuhusiana na mambo ya tolling ambayo ni lazima tuifanye kama taifa kama tutaweza kupanua barabara hizo. Kwa hivi sasa, tunajadiliana na wanakandarasi ambao watatusaidia kujenga barabara ya Rironi mpaka Mau Summit. Tutakapomaliza haya tutapitisha, kupitia Bunge hili, sheria ya tolling ili tuhakikishe kwamba barabara zetu kuu zinaweza kutupatia fedha za kutosha kujenga barabara zingine. Pia, tunataka ijengwe na wafadhili na baadaye tutaweza kuchukua zile hela ambazo zinatoka tolling kuendeleza mambo ya kujenga barabara zingine nyingi katika sehemu zingine za Kenya. Asante sana. Sen. Munyi Mundigi, hilo swali ni la maana."
}