GET /api/v0.1/hansard/entries/1421509/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421509,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421509/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kupata majibu kutoka kwa Mhe. Waziri wa Elimu kuhusiana na Katiba ya Kenya, Makala ya 189 inayozungumzia juu ya ushirikiano kati ya serikali gatuzi na Serikali ya kitaifa, imeeleza vile ambavyo serikali hizi zinaweza kushirikiana. Ratiba 4, Sehemu ya 16 pia imegawa majukumu za Serikali Kuu na serikali gatuzi. Ningependa kuelewa kutoka kwa Waziri, imekuwaje shule za sekondari na pia shule za msingi kwa sasa zinajengwa na serikali gatuzi. Imekuwaje kuwa madarasa za ECDE ama yale madarasa ya kiwango cha chini hazijengwi kabisa na serikali gatuzi na Serikali Kuu haisumbuliwi na jambo hilo. Ninataka kujua kama kuna ushirikiano kati ya Serikali Kuu na serikali gatuzi."
}