GET /api/v0.1/hansard/entries/1421847/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1421847,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421847/?format=api",
    "text_counter": 20,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo la aibu sana kutendeka katika Bunge la kitaifa. Hili ni Bunge linalotakikana kuheshimiwa. Hii ni aibu kubwa. Tangu nije hapa kuanzia 2013, hii ni mara ya kwanza kuona kitendo kama hiki kikitendeka ndani ya Bunge hili. Tungependa kujua kwa nini hakuna umeme katika Seneti. Ningependa Kenya Power itueleze kwa nini Bunge halina stima hadi saa hii. Tungependa kujua kama hatujalipa bili ya stima. Hiyo itakukwa aibu kubwa kwa Serikali. Bw. Spika wa Muda, tunataka kuwe na umeme hapa, la sivyo uahirishe kikao hiki kwa muda fulani."
}