GET /api/v0.1/hansard/entries/1421953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1421953,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1421953/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kenya inazipa Serikali za Kaunti jukumu la kuendeleza, kuanzisha, kusimamia na kudumisha vifaa vya michezo na kitamaduni ambavyo ni pamoja na viwanja, viwanja vya michezo, vituo vya kitamaduni, na miundombinu mingine inayohusiana; IKIKUMBUKWA KUWA ukanda mzima wa Pwani Nchini hauna uwanja wa kisasa uliojengwa kwa viwango vya kimataifa, hivyo kuwanyima wananchi manufaa yanayotokana na viwanja na vifaa vya michezo; WASIWASI kwamba ujenzi wa uwanja wa michezo wa Manispaa ya Mombasa umekumbwa na ucheleweshaji na vikwazo tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka wa 2019 kutokana na matatizo ya kifedha, ambayo yamesitishwa na kunyima jamii eneo hilo uwanja unaohitajika sana; KWA HIVYO SASA Bunge la Seneti linaazimia kwamba Hazina ya Kitaifa ya Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi Ubunifu na Michezo itengee Serikali ya Kaunti ya Mombasa ruzuku ya masharti ya Shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Manispaa ya Mombasa. Sasa Maseneta mnaweza kupiga kura kwa kubonyeza Ndio, La ama ususie kupiga kura."
}