GET /api/v0.1/hansard/entries/1423318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1423318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1423318/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa kuhusiana na kukataliwa na Bunge la Kitaifa kwa marekebisho ya Mswada wa Ugawaji wa Pesa za Kaunti. Ilikuwa sarakasi kubwa katika Bunge la Kitaifa jana wakati baadhi ya Wabunge walikuwa wanakejeli kazi zinazofanywa na serikali za kaunti. Tumeona kwamba pesa zilizo ongezwa na Serikali Kuu kwa kaunti zetu ni Kshs6 bilioni pekee yake. Zimetoka Kshs385 bilioni hadi Kshs391 bilioni. Lakini katika NG- CDF, Wabunge, wamejiongezea Kshs30 milioni kwa kila constituency . Ukifanya hesabu ya haraka, utapata ya kwamba NG-CDF imeongezewa Kshs8.6 bilioni. Haiwezekani kaunti zetu zinazofanya kazi kubwa, zipewe Kshs6 bilioni wakati NG-CDF inapewa Kshs8.5 bilioni. Pia tukiangalia baadhi ya gharama zimeongezeka, gharama kama vile huduma za afya, Social Health Insurance Fund (SHIF), National Social Security Fund (NSSF) na Housing Levy, hizi zote zinaongeza gharama ya kaunti kwa zaidi ya Kshs20 bilioni. Kwa hivyo, haiwezekani sisi kama Bunge la Seneti ambao tunalinda ugatuzi tuambiwe kwamba kaunti zetu hazifanyi kazi. Kila kaunti inafanya kazi. Kama kaunti yako haifanyi kazi, ni wewe na gavana wako. Kama Kiambu haifanyi kazi, ni wao na Gavana Wamatangi. Kama Murang’a haifanyia kazi, ni wao na Gavana Kang’ata. Kama Meru haifanyi kazi, ni wao na Gavana Kawira. Kama Kisii haifanyi kazi, ni Sen. Orwoba na Gavana Simba Arati. Bw. Spika, ukinunua nyanya katika soko utapata kuna zingine ambazo ni mbovu na zingine ambazo ziko sawa. Hivyo ndivyo ilivyo katika ugatuzi na NG-CDF. Kuna wananchi wanaolia kwamba hawapati huduma zozote za NG-CDF lakini kila mwaka, pesa zinakwenda kwa NG-CDF. Kwa hivyo, nawasihi wenzangu ambao tutachaguliwa katika--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}