GET /api/v0.1/hansard/entries/1423325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1423325,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1423325/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, ninawaomba wale tutakaowachagua; wakienda pale kuzungumzia ugatuzi na kuwatetea magavana wenye shida ya pending bills na wage bill, wawe wamejikakamua kabisa wasiwekwe chini na hao watu. Ni aibu sana MP ambaye hafanyi kazi kusema kwamba gavana hafanyi kazi. Ninaunga mkono kuwa wale watakaoenda kututetea, wawe na ushujaa na kutuletea pesa. Tunafahamu kuwa mwaka uliopita tuliwapa magavana pesa ambayo haikutosha hadi kaunti hazikufanya ile kazi ya ugatuzi tunayotaka. Majukumu ya kaunti ni hospitali, maji na kuwasaidia watu kona zote. Watakaoenda kututetea waende kama Bunge la ‘Juu’ na wasiwekwe chini na wale MPs wanaotaka kula pesa. Kila MP ametengewa Kshs150 milioni. Kila MP amepewa pesa ya barabara Kshs50 milioni na hatujui zinafanya kazi gani. Hatukatai kazi yao ni kupeana basari ya shule. Hiyo nyingine ni kujengea afisi za DC. Ni aibu kubwa sana kwamba zile pesa zinazoenda kusaidia mwananchi ambaye amelipa ushuru, MP anasema gavana hafanyi kazi. Nawaambia MPs wote kuwa hakuna yeyote anayefaa kumunyooshea gavana kidole. Angesema sisi maseneta ndio tunaofaa kufanya hiyo kazi. Asante. Naunga mkono."
}