GET /api/v0.1/hansard/entries/1424205/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424205,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424205/?format=api",
    "text_counter": 629,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, tumeona watu wengi waliozaliwa vizuri wakiwa na mikono, macho na pia walilelelwa na kufunzwa vizuri na familia zao. Cha ajabu ni kwamba, wakati tulikutana na hao, wengine hawakuwa na miguu au macho. Wengine wana elimu ya juu lakini kwa sasa, ni maskini hohe hahe. Kwa hivyo, naomba Kamati iweze kusaidika. Wakati Kamati ya watu tisa ilitengenezwa, tulikuwa na mipango ya kwenda USA. Cha ajabu ni kuwa, Kamati ilikosa pesa. Ni watu wawili pekee ndio waliweza kusafiri. Hii ni kama hakuna kitu Kamati inafanya. Ndio maana tunasema, wale wanaohusika na mambo ya pesa, waongezee Kamati pesa ili ziweze kufanya kazi inayofaa. Juzi, tulikuwa tukisema kaunti zipatiwe Kshs415 bilioni. Lakini, Members of Parliament (MPs) walipinga. Naomba Kamati zote ziongezewe pesa ili ziweze kufanya kazi inayofaa kwa sababu tunajua Kamati za Senate hazina mambo mengi. Tunataka kusaidia wananchi vijijini, kaunti na Kenya mzima. Kwa hivyo, naunga mkono. Lakini, kama Kamati zingine zinateseka kama Kamati ya Ad Hoc kwa sababu ya ukosefu wa pesa ya kufanya kazi, ni aibu sana. Tumekuwa tukifanya kazi kwa miezi kadhaa bila pesa, tumejitolea tu. Naomba tuongezewe pesa ili Kamati iweze kwenda USA ili tushughulikie vilivyo hawa watu. Pia zile departments zote tulizohusisha kama vile Health, National Administration na Laborand Social Protection ziweze kupewa kitu kidogo. Naunga mkono. Asante Bi, Spika wa Muda."
}