GET /api/v0.1/hansard/entries/1424293/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424293,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424293/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ningependa kuongezea yale maneno Mhe. Mungatana amesema. Mhe. Mungatana ametoka Kaunti ya Tana River na labda amesafiri usiku wote akifikiria kwamba leo asubuhi atawakilisha watu wake wa Tana River. Lazima tukubaliane kama Seneti kwamba Waziri hataweza kufika kama labda ni mgonjwa au ameitwa State House kwa mkutano muhimu sana. Tukubaliane kwamba Waziri yeyote ambaye atashindwa kufika hapa kwa sababu ya safari ambayo mipango yake ilianza miezi miwili iliyopita, ingefaa atume msaidizi wake kama vile PrincipalSecretary . Waziri ambaye hajafika leo ni kama hajali maneno ya Bunge. Hii ni kwa sababu wakati alifika mbele ya Bunge kwa ajili ya mambo ya fertilizer, nilimwambia ajiuzulu kwa sababu responsibility ya kuhakikisha kwamba wakulima wanapata fertilizer kwa bei nzuri na wakati ufaao, ni yake. Wakulima walikosa fertiliser kwa wakati unaofaa. Pia walipata fertiliser gushi. Bw. Spika, tungeleta Censure Motion kwa huyu Waziri. Ingawa ameachiliwa na Bunge la Kitaifa, bado maneno yapo. Ukitazama poll sasa hivi, karibu asilimia 99 wanasema huyu mtu aende nyumbani. Ako na heshima gani kuongoza nchi hii kama Waziri wa Kilimo? Bw. Spika tunakuomba tukubaliane kuwa ikiwa Waziri atashindwa kufika mbele ya Seneti iwe tu kwamba ni mgonjwa au ameitwa State House katika shughuli ya kuzungumza na Rais wa nchi hii. Mambo mengine yote ni njia ya kuchelewesha mipango ya serikali, Seneti au Bunge. Asante sana. Ni vizuri tuchukue hatua ya kusaidia nchi isonge mbele."
}