GET /api/v0.1/hansard/entries/1424327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424327/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gataya Mo Fire",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, swali langu linaambatana na swali la msingi. Ninakumbuka mwezi moja ama miezi miwili iliyopita, tulifanya msafara pamoja na Wariri wa Maji hadi sehemu za Tharaka-Nithi. Kaunti ya Tharaka-Nithi ni kaunti ambayo imekumbwa na matatizo makubwa ya maji, sanasana, sehemu ya Tharaka Constituency. Ninakumbuka tulitembelea sehemu za Marimanti pamoja na Waziri ambapo kuna miradi kadha wa kadha ambayo imeanzishwa na wenyeji wa maeneo hayo. Kuna Mradi wa Kathura Water Project ambao unasambaza maji mpaka Marimanti, mpaka sehemu za Maragwa, Tharaka North. Kuna mradi mwingine unaoitwa Sisi kwa Sisi ambao uko sehemu za Mukothima. Kuna Mradi unaoitwa Mukithi Water Project, ambao unashughulikia sehemu za Muwii mpaka Kithioroka. Kuna Mradi unaoitwa Magatianthe katika sehemu za Marimanti ambao unashughulikia sehemu za Rungu na Murinda katika Ciakariga Ward. Vile vile, kuna Mradi uitwao Kiramanti katika Marimanti."
}