GET /api/v0.1/hansard/entries/1424343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424343,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424343/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Namshukuru Waziri kwa kuchukua nafasi hii kujibu maswali. Swali langu ni kuhusu mkopo uliotolewa na benki. Kuna bwawa kubwa Kaunti ya Nandi linaloitwa Keben lilioanzishwa miaka kadhaa iliyopita. Vile vile, kuna bwawa lingine linaloitwa Kipkaren kwenye mpaka wa Kaunti za Uasin Gishu na Nandi. Swali langu linahusiana na mkopo uliokopwa na Serikali kutoka African Development Bank (ADB) . Kuna muda uliowekwa na benki hii inayofadhili mradi huu wa kujenga bwawa la Keben kwenye eneo Bunge la Nandi Hills. Ni muda gani utatumika kukamilisha mradi huu na ule wa bwawa la Kipkaren lilioko kwenye mpaka wa Kaunti za Nandi na Uasin Gishu ili wakaazi wa Kaunti ya Nandi na Uasin Gishu wapate maji safi ambayo watatumia nyumbani na kilimo? Kilimo ni uti wa mgongo wa Kaunti ya Nandi. Ningependa Waziri ajibu na kutupa hakikisho kuwa miradi hii itakamilika wakati unaofaa. Mkopo kutoka African Development Bank ukipatikana, kutengeneza na kumaliza mabwawa haya mbili itakuwa rahisi."
}