GET /api/v0.1/hansard/entries/1424349/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424349,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424349/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Karibu Waziri. Swali langu ni kuhusiana na mradi wa climate resilient ambao ulifanyika Likoni Sub-County. Ni jambo la kusikitisha na kutamausha ya kwamba, tangu mradi huo ulipofanyika miaka sita nyuma, hadi leo haujafunguliwa. Watu wa Likoni hawajaanza kupata maji safi. Hivi leo watu wa Likoni wananunua maji yanayoitwa Malele, dumu moja kwa Kshs40. Mimi kama mwanamke, najua umuhimu wa maji. Asubuhi tukiamka tukitaka kufua tunatumia maji. Wanaume wetu wakitaka kwenda kazini lazima tuwawekee maji ya kuoga. Kwa niaba ya watu wa Likoni, nakuomba utueleze kwa nini Serikali iliwekeza pesa nyingi, mradi ukafanywa lakini mpaka leo watu wa Likoni wameshidwa kupata maji safi ya kunywa kwenye mifereji ndani ya nyumba zao."
}