GET /api/v0.1/hansard/entries/1424400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424400,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424400/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gataya Mo Fire",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, kuna watu ambao wanazungumza hapa. Tumekuwa na Waziri kwa muda mrefu na tumekubaliana mambo mengi kuhusu sehemu kame zilizoko Tharaka-Nithi. Kuna mito mingi na tulipanga kutakua na madimbwi na mabwawa na vile vile, tutachimba visima zile sehemu za chini kule Tharaka hakuna mito. Tuliweka pia mikakati na watu wakaja wakapima visima lakini, tumemaliza mwaka mmoja. Hatujaona kama kuna mipango yeyote ya Serikali na sijui kama hio mipango iliachwa ama bado iko. Ningependa kujua ni mikakati gani Wizara yake imetia. Bw. Spika, ukienda sehemu kama za Gatunga, kule Maragua, wakati mwingi, watu hutumia maji na wanyama. Unapata mnyama anakunywa maji na binadamu pia, anakunywa yale maji---"
}