GET /api/v0.1/hansard/entries/1424490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424490/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gataya Mo Fire",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Naibu Spika. Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Waziri kwa sababu amedhihirisha ufasaha na ustadi wa hali ya juu katika Wizara yake. Vile vile kwa maswali ya ziada ambayo yamemjia kabla ya kujitayarisha. Ameonyesha ya kwamba ana ustadi wa kutosha. Waziri unakumbuka hivi kwamba miezi sita iliyopita, ulisafiri mpaka Kaunti ya Tharaka-Nithi. Nimesikia ukitaja pahali panapoitwa Kithiori. Isipokuwa umeitaja kujuuju, ulisafiri mpaka mahali panapoitwa Maragwa iliyoko Tharaka North. Vile vile ukasafiri mpaka Kithiori ambayo ina historia ndefu sana ya madini. Watu wa Kaunti ya Tharaka-Nithi mpaka sasa hivi, hawajapata ripoti kuhusu safari yako ni nini mliona na ni nini mmepanga kufanyia watu wa Tharaka Nithi. Bw. Waziri, eleza kama madini haya yana umuhimu wowote wa kiuchumi na ni mikakati gani ambayo watu wa Kaunti ya Tharaka Nithi wana arajia kuona? Juzi kumekuwa na walaghai ambao walikuja bila idhini ya viongozi wa kisiasa na walifurushwa. Waziri, watu wa Kaunti ya Tharaka-Nithi wangependa kujua Wizara yako inafanya juhudi gani kuhakikisha madini yaliyoko kwenye sehemu za Kithiori, Maragwa na mahali pengine kwenye kaunti hii inawafaidi."
}