GET /api/v0.1/hansard/entries/1424530/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424530,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424530/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Swali langu linahusu uchumi samawati, chini ya ile programme ya Waziri ya Kenya Marine Fisheries Economic Socio-Development Project (KEMFSED). Kwanza, nashukuru Waziri kwa kazi anayoifanya kwa sababu sisi tumeikubali na Wakenya wameikubali pia. Waziri alikuja kwetu Tana River na ukatueleza kwamba kuna vijana wanaotakikana kwenda wakafanyiwe masomo ya coxswain. Alisema utawalipia haya masomo na kweli, vijana 12 kutoka Kipini walienda. Saa hizi wako Kisumu. Katika makubaliano, ilikua kila siku wanalipwa Kshs4,000 ili wapate mahali pa kulala, nauli na chakula. Siku 30 zimepita na kukawa sawa maanake waliambiwa, masomo yatakua siku 45. Lakini, zile siku 15, Kizungu, Kiingereza na Kichina vikaingia sasa. Wanaambiwa eti sasa pesa ni Kshs1,000. Bi. Spika wa Muda, vile ninavyoongea na Bw. Waziri, jana, vijana wangu 12 walikataa kwenda masomoni kwa sababu hakuna nauli, chakula na mahali pa kulala ni shida pia. Je, Bw. Waziri anaangalia haya? Kuna wizi unaendelea kwa program yake nzuri ambayo ameianzisha. Ningetaka atwambie hii mipango ya kuambiwa ni Kshs4,000 halafu inageuzwa inakua Kshs1,000 ni kweli, ni sawa na ni haki? Mtu ataishi hivyo namna gani? Ninaomba Bw. Waziri akitoka hapa, afute kazi mtu kule Tana River kwa Fisheries, maanake ni lazima watu waonyeshwe ya kwamba, hatutaki wizi, ufisadi na utapeli kwa wananchi wa kawaida. Watoto wadogo wanaenda kutafta elimu ili wasaidike halafu inakuwa namna hii. Swali langu ni, je, ni hatua gani atachukua kusaidia watoto wetu wa Kipini, Tana River?"
}