GET /api/v0.1/hansard/entries/1424532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424532/?format=api",
    "text_counter": 280,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Natoa shukrani kubwa kwa Waziri wetu wa Madini. Kuna viongozi wengi hapa wana hamu ya kusikia na kama Seneta wa Jimbo la Kaunti ya Kwale nitagusia ile madini yanayochimbwa na Base Titanium. Hili shirika liko karibu kufunga na kuondoka katika ile migodi wanayochimba kule Kwale. La kwanza nikutoa shukrani kubwa kwa Waziri kwa sababu wiki iliyopita, tulikua pamoja naye Kwale na mdogo wake na viongozi wengine katika Wizara yake. Kulikua pia na Wabunge, Maseneta na Viongozi wa Wadi kutoka Kwale. Namshukuru pia kwa kuzindua kamati ya Coast Mining Committee ambayo mimi kama Seneta wa Kwale natoa shukrani kwa kuchagua hii Kamati. Hii Kamati imejumuisha viongozi kutoka serikali ya kaunti ya Kwale. Sisi viongozi tulio na nadhifa za ubunge, seneta na madiwani tumepewa fursa ya kuweka watu kwa ile Kamati."
}