GET /api/v0.1/hansard/entries/1424543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424543/?format=api",
    "text_counter": 291,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Waziri, kuna wakati ulitembea Embu. Ulienda Mbeere South kwa mlima unaoitwa Kiangongoro na ukapata dhahabu ambayo inaweza kusaidia economy ya Embu County. Pia, uliongea mambo mazuri sana ya kusaidia Wambeere ambao wanaishi kwa huo mlima na tulifurahia sana. Vile uliona, hiyo area imewachwa nyuma kwa maendeleo. Pia, tulifurahia kwa sababu katika bajeti ya Kenya, upande wa dhahabu, ulipea Kaunti ya Embu Kshs2 milioni ambayo ni pesa kidogo sana. Kwa bajeti inayokuja, unatupangia nini watu wa Embu ili pia sisi tufurahie hiyo pesa ya dhahabu? Pili, nakuomba wakati utakuwa ukitembea kwa kaunti, uwe unahusisha Maseneta. Mimi ni Vice-Chairperson, Committee on Agriculture, Livestock and Fisheries. Lakini, uliwacha vita kwa wale wako kijijini. Walibaki wakiuliza kwa nini sikuonekana ilhali mimi ni mtetezi wa watu wa Kaunti ya Embu; Wambeere na Waembu. Naomba wakati unatembea kwa Kaunti, ufanye kazi na Maseneta. Hawatakuangusha---"
}