GET /api/v0.1/hansard/entries/1424558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424558,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424558/?format=api",
    "text_counter": 306,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "Asante Bi. Spika. Kwanza nachukuwa nafasi hii kumshukuru Waziri na Principal Secretary (PS) wake. Tulikuwa na shida ya mining Moyale, tukapiga simu na tukawapata. Tunawapa shukrani kubwa sana. Bi Spika wa Muda, kuna migodi Moyale inayoitwa Hilo. Inasaidia watu 5,000. Hivi majuzi hiyo migodi imefungwa kwa sababu ya watu kupoteza maisha yao. Ningependa kujua kutoka kwa Waziri; ni hatua gani anachukua kwa sasa kwa sababu watu wanaoishi Moyale, Marsabit na Isiolo wanategemea hiyo migodi. Ni kweli watu walifariki pale na ikafungwa? Ni hatua gani unachukua? Hawa watu wa migodi wamekubaliana wakaketi na kutengeneza cooperatives ya kufanya hiyo kazi kwa njia inayokubalika kisheria. Waziri atueleze ni lini ataketi na hao watu ambao wametengeneza cooperative ili tupate nafasi kama viongozi pia tuketin nao. Waletwe pamoja ndio hiyo sheria ya kufanya hiyo kazi iende katika njia inayotakikana."
}