GET /api/v0.1/hansard/entries/1424562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424562,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424562/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda. Yangu yatakuwa ni maoni nikiongea kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima, Uvuvi, Mifugo na Uchumi Samawati. Kati ya maswali ambayo yanaulizwa hapa kama Kamati tungeweza kujibu. Kwa hivyo, ningetaka niseme kama Mwenyekiti kwamba nasikitika kidogo kwa sababu mialiko ambayo tumekuwa tukifanya sikuona Katibu wa Kudumu Katika Wizara ya Uchumi Samawati. Ningeomba, tunapoitana tena waje kwa sababu katika shughuli muhimu na maswali yanayoulizwa na Seneti ambayo ni muhimu, tumeshindwa kujibu kwa wakati tunaopewa kwa mujibu wa sheria na Kanuni za Kudumu za Seneti kwa sababu ya kukosa kuwajibika na kuwaona katika Kamati ya Ukulima. Hilo nimeongea kwa kusikitika lakini tunaunga mkono, na asante kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya. Asante."
}