GET /api/v0.1/hansard/entries/1424566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1424566,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424566/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nazungumza hivi nikigongelea msumari mazungumzo ya Sen. Boni Khalwale. Tuko na wafanyibiashara wengi kuanzia Vanga hadi Kiunga. Tunapovuka kivuko cha Likoni, kuna wamama wengi pale wanauza samaki. Sen. Veronica alipokuwa anaongea, amezungumza yale yaliyokuwa moyoni mwangu. Nimezungumzia maswala ya wanawake kwa sababu, mahali popote panapo zungumziwa kijana mwanamke ama mtu yoyote yule anayeishi na ulemavu, huwa kunaingia firfinyange. Hadi wa leo wale wanawake wanaojihusisha na biashara ya kuuza samaki yaani wale wachuuzi wanaopika, kukaranga na kuuza rejareja. Pamoja na wale wengine ambao wako kando pale Likoni katika kivuko. Hawajafaidika na mradi wa aina yoyote katika Wizara ya Uchumi Samawati. Waziri nakuomba na nimekuita hapa kwa sababu moja. Kesho utakapoondoka katika hicho kiti, watu wa Pwani wasiseme mtoto wetu alikuwa amekaa hapo na hakutusaidia. Ndiposa nikakuuliza je, kuna sheria inayokuzuia wewe kutokusaidia jamii ya Wapwani ambao wanazingatia sana na kutarajia uvuvi kama uti wa mgongo? Sisi hatuna mashamba mengine ---"
}