GET /api/v0.1/hansard/entries/1424589/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424589,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424589/?format=api",
"text_counter": 337,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Salim Mvurya",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Mining and Blue Economy",
"speaker": null,
"content": "regulations that I have put forward before this House have also created an enabling environment that will protect women. Later this year, we will have a whole conference with the Common Market of East and South Africa (COMESA) and other countries to discuss this matter in great detail, so that we can also get much more commitment to the protection of women. Sen. Chute from Marsabit, thank you very much. We indeed closed the Dabel. Bi. Spika wa Muda, naona hii swali imeulizwa kwa Kiswahili na wakati mwingine hii sekta yangu inakosa misamiati. Tulifunga Dabel sehemu ya Marsabit kwa sababu kulikuwa na mambo mengi ya uchimbaji migodi bila leseni kwa hivyo tukafunga. Hivi sasa tayari tumesajili vyama vya ushirika sita kwa sababu nia yetu ni kwamba wananchi wa kawaida wakiwa kwa vyama vya ushirika, wataweza kuwa na nafasi pia ya uchimbaji migodi pamoja na wale waekezaji wakubwa. Wakati huu tuko kati shughuli hiyo na tumewasajili. Tutatembea tena twende tuangalie hiyo sehemu ndio tutengee sehemu ya ushirika na uwekezaji mkubwa. Hizi ni shughuli ambazo tutazifanya tukishirikiana na nyinyi kama viongozi na sekta zingine za serikali kuhakisha pia kuna usalama wa kutosha. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo tunalitilia maanani na tunataka kuendelea kuhakisha tumeweza kuwa wabunifu katika sekta hii, na pia wananchi wa kawaida ambao wamekuwa wachimbaji migodi waweze kufaidika. Jambo lingine muhimu ni usalama haswa katika ufuo wa bahari ambayo pia imeguziwa. Katika mambo ya usalama tunafanya kazi na vitengo vya usalama, CoastGuard na vitengo vingine vya jeshi letu kuhakisha kwamba Bara Hindi iko salama. Hii ndio maana mwanzo wa mwaka jana Bara Hindi iliweza kutolewa katika ile hesabu ya zile fuo za bahari ambazo ni hatari na ikasemekana sasa iko na usalama wa kutosha. Kwa hivyo, ni jambo ambalo tumechukulia maanani na tunatangazia kila mtu ya kwamba, Indian Ocean iko salama. Hii ni kwa sababu hapo Indian Ocean, mbali na kwamba tuna jeshi letu, Coast Guard na vifaa muhimu tumepata ambavyo vimegharimu Kshs3,600,000,000. Bi. Spika wa Muda, pia tuna tugboats mpya ambazo zitazunguka na maafisa wetu ili kutela usalama katika ufuo wa bahari. Pia, tunajenga kituo hapo Mombasa na Ziwa Victoria ya search and rescue . Tutatumia teknologia ili kuhakikisha kwamba tunajua mahali usalama umekosekana. Mwezi wa Disemba, tulishirikiana na vyombo vya usalama ili kuona kwamba tunawanusuru wale mabaharia na wavuvi ambao walikua wamepotea na baadae wakarudi nyumbani. Hii ni kwa sababu ya hivi vifaa ambavyo tumeweka ili kuleta mambo ya usalama. Bi. Spika wa Muda, nachukua nafasi hii kusema kwamba hizi sehemu nyingi za bahari, maziwa na mito, haswa wakati huu wa mafuriko, ni muhimu watu wawe waangalifu. Tumeona sehemu nyingi kama Baringo mahali kuna boti ilikua na watu wengi zaidi ya kipimo. Kwa hivyo, wananchi wajihadhari."
}