GET /api/v0.1/hansard/entries/1424591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1424591,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1424591/?format=api",
"text_counter": 339,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Salim Mvurya",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Mining and Blue Economy",
"speaker": null,
"content": "Mwisho kabisa kwa swali limeulizwa na Sen. Miraj na amezungumza moyo wake safi kwa ufasaha kuhusu vile kina mama wanashiriki kwa biashara ya samaki na uchumi samawati. Mbali na hii bilioni moja ambayo tumezungumzia inaangaliwa na sekta ya kibinafsi, kuna mradi mwingine tunashirikiana na Benki ya Dunia na ruzuku zingine zinavyofaidi vikundi vingine. Bi. Spika wa Muda, Mheshimiwa Rais mwaka jana alipeana Kshs320,000,000 na baadae akapeana Kshs700,000,000 na hivi sasa tuko na Kshs1,200,000,000 ambayo iko tayari kwa akaunti zile. Tunatakiwa tufanye kazi na kaunti. Wananchi wanatakikana watume maombi kwa kaunti, watuletee yale maombi wamepitisha ili tuyaangalie hapa, tuwaandikie cheki na tuwatumie pesa ya kufanya biashara yao. Hii ni nafasi nzuri ya kuhimiza kushirikiana vizuri ili tuhakikishe wengi wamefaidi. Kwa muda huu ambao tumefanya kazi na nyinyi, kumekua na uwazi na kwa hivyo, tunataka kwendelea kushirikiana na wale mama wa samaki ili waweze kufaidika na yale yote tunayapangia. Bi. Spika wa Muda, kwa hayo mengi na kwa sababu ya muda, nitakomea hapo. Nitasema pia kikao kama hiki ni kizuri. Nimeona yule Seneta ameuliza mambo ya katibu na Katibu wa Blue Economy ako hapa na anapitakana wakati wote, na kama kuna habari zinatakikana kuelezana, hata mimi nitafika kuwaeleza. Mungu awabariki na asanteni sana."
}