GET /api/v0.1/hansard/entries/1425089/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425089,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425089/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu wa Spika, nikiwa Seneta wa Embu Kaunti, naunga mkono kamati ambayo imetengenezwa inayojumuisha Maseneta kutoka upande wa walio wengi na walio wachache. Ni kamati ya watu mashujaa, walioelimika vizuri na wameona matatizo yaliyoko katika kaunti zetu 47. Hii haimaanishi kwamba Maseneta wengine hawawezi kufanya kazi hiyo kikamilifu. Najua tuko Maseneta 67. Lakini, hiyo kamati iko na Seneta wa Kaunti ya Meru, Sen. Kathuri na Sen. M. Kajwang’, Seneta wa Nairobi Kaunti na wengine mashujaa. Ningeomba waende wazungumze na watulutee matunda kwa sababu katika kaunti zetu zote 47 mambo ya devolution yameleta shida. Kaunti nyingi, kwa mfano, Embu haipati pesa za kutosha ilihali magavana wanataka pesa nyingi."
}