GET /api/v0.1/hansard/entries/1425171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425171,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425171/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa hii kuhusu Siku ya Kimataifa ya Chai iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey. Mombasa ndio soko kubwa kabisa la chai ulimwenguni. Ni faraja kubwa kwa watu wa Mombasa kwamba kwa miaka mingi sasa, wamekuwa wenyeji wa soko la chai ulimwenguni. Sio chai ya Kenya pekee ambayo inauzwa katika soko la chai la Mombasa. Kuna chai kutoka Burundi, Rwanda, Tanzania na sehemu nyingi ambapo chai hizo huchanganywa na chai ya Kenya – kwa sababu chai ya Kenya ni bora zaidi – ili kuboresha chai zingine ambazo zinauzwa ulimwenguni."
}