GET /api/v0.1/hansard/entries/1425173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425173,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425173/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi karibuni kumekuwa na hujuma ya soko la chai katika Kaunti ya Mombasa. Hujuma hizo zimechangia mataifa mengine kufungua masoko yao ya chai. Kwa mfano, nchi ya Tanzania imefungua mnada wao wa chai. Chai yao haiji tena Kenya kwa sababu ya masuala kama haya ambayo ninayazungumzia. Tunapozungumzia jinsi ya kusaidia kuinua uchumi wa chai, ni lazima tuangalie pande zote mbili. Chai bila soko haitaweza kusaidia mkulima. Lazima chai ipate soko bora ambayo itaweza kumsaidia mkulima na yule ambaye anauza chai hiyo. Hapa katikati kuna Shirika la Kenya Tea Development Agency (KTDA). Juzi tulikuwa na mkutano wa Kamati ya Labour and Social Welfare ambapo kuna suala lililotokea. Shirika moja la chai ambalo linaajiri wafanyikazi limekataa kulipa mfanyikazi kwa muda wa miaka mitatu sasa. Viongozi wa KTDA walipoitwa kuja mbele ya kamati yetu, walisema kwamba huyo sio mfanyikazi wao ilhali kampuni ya chai ambayo inahudumu kule inasema huyo ni mtu wao. Mara nyingi, mashirika kama KTDA ndio yanahujumu juhudi za mkulima. Katika soko la chai la Mombasa, wengi wanatumia wakati wao kufanya utafiti ili kuboresha chai. Kwa mfano, wiki iliyopita, niliwaambia baadhi ya Maseneta watumie chai ya hibiscus ambayo ni mojawapo ya chai ambazo zimebuniwa. Siku hizi kuna ladha tofauti tofauti za chai ambazo zinauzwa. Hii inachangia pakubwa kuipa Kenya fedha za kigeni. Tunaposherehekea Siku ya Kimataifa ya Chai, ni lazima pia tutambue mchango unaofanywa na Shirika la East African Tea Trade Association (EATTA) kule Mombasa pamoja na soko la chai la Mombasa kwa sababu pale ndipo wale wanaonunua chai wanakutana na wale wanaouza ili kuhakikisha kwamba soko la chai linaendelea kupanuka."
}