GET /api/v0.1/hansard/entries/1425186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425186,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425186/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Ninaunga mkono siku ya kesho ya wakulima wa majani chai. Katika Kaunti ya Embu tuko na kaunti ndogo nne na Manyatta na Runyejes hupanda majani chai. Mambo ya maajabu ni kuwa miaka mingi wamekuwa wakipanda majani chai. Wakati tulizaliwa, tulikuta watoto wakiripiwa karo na pesa za majani chai. Lakini, wakati huu kuna aibu kubwa sana. Hii ni kwa sababu, kilimo cha majani chai kinaendelea kuzoroteka na bei inaendelea kwenda chini. Wakiendelea na siku ya kesho, wataongea vile kilimo cha majani chai kifaa kuchukua ile njia inafaa ili bei iweze kuimarika na kusaidia wakuliwa wa majani chai. Kama kuna mtu anaumia ni mkuliwa wa majani chai. Yeye huamkwa saa kumi na moja wakati mvua inanyesha. Hawa ni wazee, akina mama na watoto."
}