GET /api/v0.1/hansard/entries/1425188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425188,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425188/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Wakati wa kuchuna majani chai na kuuza, wakulima hawa huwa na hasira nyingi sana. Ninaunga mkono hii siku na pia bei iangaliwe. Barabara katika maeneo ya majani chai huwa hazipitiki. Magari mengi hukwama. Hizi barabara zinaweza kuimarishwa kupitia NG-CDF. Bw. Naibu wa Spika, ningetaka kukosoa Sen. (Prof.) Kamar kwa kutaja mambo ya muguka na miraa. Upande wa Mashariki wa Mlima Kenya – Embu, Meru na Tharaka Nithi, hii mimea ni kilimo yetu kutoka zamani. Watu wa chini walikuwa masikini lakini kwa sasa, tungetaka kuwe na value addition, ili tuweze kutengeneza juisi, gamu ya kutafuna na vitu vinginevyo. Ningeomba huyu Seneta ile wakati tutaleta huu Mswada hapa, vile nimekuwa nikisaidia kuunga mkono miswada yao, pia wao wanisaidie tufike Maseneta 27 au 30. Ningetaka kumwambia Sen. (Prof.) Kamar tena kuwa muguka na miraa ilikuweko kutoka zamani za mababu wetu. Ni mimi, Deputy Party Leader, Alexander Munyi Mundigi."
}