GET /api/v0.1/hansard/entries/1425222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425222/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Wengi wametaja na kusifia kubugia aina nyingi ya chai. Lakini katika kizazi hiki cha Serikali ya Kenya Kwanza, japo tunasherehekea siku ya kimataifa ya chai, ni lazima tuhakikishe kwamba katika vitongoji vya nchi hii wakulima na wanywaji wa chai wanajivunia vinywaji hivi. Bw. Naibu Spika, katika bonde la ufa na sehemu ya Mlima Kenya miundo mbinu na msingi imewekwa imara ili kuwalinda wakulima pamoja na viwanda vya majani chai. Katika Mkoa wa Magharibi mambo ni tofauti. Japo tunasherehekea kimataifa, kimashinani watu wana maswali ya kuuliza. Katika mkoa huu, hususan Mlima Elgon na vitongoji vya kaunti ya Bungoma, tulikubaliana na Serikali kwamba ni lazima au ni sharti kuwe na viwanda au kiwanda ili wakulima wa majani chai katika eneo hilo wafurahie kama wenzio kutoka sehemu mbalimbali za nchi ya Kenya. Hadi sasa, mfumo wa makadirio ya kifedha umepita lakini bado tunaishi kwa matumaini. Tunataraji kuwa isiwe hadithi ya matumaini ya mbwa kutamatika pale ule mlango wa jikoni unapofungwa. Sasa, tunajadili umuhimu au ubora wa majani chai lakini hatuwezi kuwa na majani chai ya hali ya juu iwapo pembejeo ni gushi na watu wanaohusika hawawajibiki wala kuhakikisha kuwa wakulima wa majani chai, pareto na kahawa wanapata mbolea ambayo inastahili na hivi kwamba ni ya kiwango cha kimataifa. Japo tunafurahia haya, kama Serikali tuna changamoto kuhakikisha kwamba tunaendelea kufurahia kwa pamoja kwa jasho la haki. Wasio wakulima wanatoa jasho, na wachache wanakula manufaa ya jasho la wakulima katika nchi ya Kenya. Sasa, ni jukumu letu sote kama Maseneta katika Bunge hili kuhakikisha kuwa tunawatendea haki wakulima, wanywaji wa chai na vile vile washika dau katika sekta nzima ya chai. Asante sana. Nawatakia sikukuu njema ya chai."
}