GET /api/v0.1/hansard/entries/1425315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425315,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425315/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "karo ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Ingawaje, tunaunga mkono hiyo kazi. Kazi nyingine ya hizo pesa ni kutengeneza barabara. Wamekuwa wakipigana na kusema kwamba wanafanya kazi zote. Ni aibu kubwa sana kwa sababu sisi kama Maseneta hatuangalii kazi wanayoifanya. Tukipeleka Miswada yetu, wanatuangalia kwa macho mabaya. Kwa hivyo, yale mambo wanayosema kuhusu huu Mswada ni ya aibu. Tunajua ugatuzi ulikuja ili mwananchi aliye mashinani aweze kufaidika. Kwa sasa, wanataka kuturudisha kule tulikotoka miaka iliyo pita. Kwa hivyo, napinga. Wanafikiria kuwa wanatembea mbinguni wengine wetu tukiwa huku duniani. Nawaambia kuwa sisi sote tuko hapa ulimwenguni na wakati wa kwenda mbinguni, Mungu atakuja kutuchukua. Jambo la pili ni kuwa wiki jana nilimsikia Mbunge mmoja akisema kwamba ati pesa ya MCAs ikipitishwa, iwekwe kwa NG-CDF. Hii ni aibu kwa sababu hata hawana heshima kwa MCAs. Waheshimiwa Wabunge wa National Assembly wanaleta aibu. Hatuna haja na kazi zao na wasisikie vibaya kutuhusu. Pengine kile kitu kinacho tuunganisha ni mshahara tu. Kutoka leo, ninawaambia kuwa tuko Maseneta 67, 47 wanaongoza kaunti 47 na 20 wameteueliwa na vyame mbalimbali. Tunaangalia vile magavana wanafanya kazi na tumeona wanafanya kazi inayofaa. Ndio maana wiki jana, tulisema serikali za kaunti zipatiwe shilingi bilioni 415, ili watu wafanyiwe kazi ya kutosha katika ugatuzi. Magavana kule vijijini wana kazi nyingi. Ndio maana tunawatetea waongezwe pesa. Wako na kazi kama vile ya kilimo, afya, maji na mambo mengine ili mfanyikazi na watu kijijini waweze kujisaidia kwa sababu wanalipa ushuru. Ni aibu kubwa sana kuwa Wabunge wanatuchokoza ilhali hatuna haja na pesa zao na hatujawachokoza. Waliotengeneza Katiba na kusema kuwa Maseneta wawe ‘Bunge Kuu’ walikuwa na akili ya kutosha. Wao waliangalia vile mwananchi alivyokuwa akiteseka. Ndio maana ugatuzi ulikuja na sisi tunafanya kazi inayofaa. Pia, walitunyima pesa hata ya mradi wowote ili tuweze kuangalia kazi kule vijijini. Bw. Spika wa Muda, hawa Wabunge wamezoea vibaya sana. Ukienda kaunti zingine wakati kuna mkutano wa Raisi au gavana, Wabunge wanapewa muda mrefu wa kuongea lakini Seneta haheshimiwi hata na naibu wa gavana. Naomba Kenya nzima itafsiriwe kiwango cha Seneta. Kulingana na Katiba katika mikutano Seneta anahitajika kuzungumza kwanza, kisha MP, Women Representative, gavana na mwisho naibu wa gavana. Kwa hivyo, Maseneta wanadharauliwa lakini wanafanya kazi ya kutosha ya kuangalia vile gavana anavyofanya kazi. Ningeomba wakituingilia hivyo, sisi pia tupitishe sheria itakayohakikisha pesa za NG-CDF zinakaguliwa ipasavyo. Wanajipiga kifua kwa sababu hakuna mtu ana uwezo wa kukagua pesa hizo. Ni aibu kubwa sana kwa hawa MP kutudharau, lakini watajua kuwa sisi ni ‘nyumba ya juu’ na wao wako kwenye ‘nyumba ya chini.’ Kwa hivyo, naomba turudi kwa Katiba tena ili tujuwe vile kuko, kutoka kwa MP, Women Representative, Seneta halafu gavana. Kuna Maseneta hawawezi kuongea hapa kwa vile wamenyanyaswa na MPs. Ndio maana tumepitisha vile tutakuwa tunafanya."
}